Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar waanza kuwajengea uwezo Watanzania wanaoajiriwa huko

Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar umeanzisha rasmi programu ya mafunzo kwa waajiriwa wapya kutoka Tanzania wanaokwenda kufanya kazi nchini humo, anaripoti Mwandishi Maalum Diramakini (Doha).
Bw. Sahim Ayoub Khatib (mwenye karatasi), Diaspora wa Tanzania nchini Qatar ambaye pia ni mwajiriwa wa Kampuni ya HBK ya nchini humo akitoa mafunzo kwa Mabinti 9 kutoka Tanzania ambao wameaajiriwa na Kampuni ya Manpower Solutions (WISA) inayomilikiwa na Serikali kwa ajili ya kufanya kazi za usafi na huduma za ndani. Mafunzo hayo ambayo yanalenga kuwajengea uwezo pamoja na kuwaelewesha sheria na taratibu za ajira za Qatar, yameandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini humo. Mafunzo hayo yalifanyika kwenye Ofisi za Ubalozi hivi karibuni na kusimamiwa na Bw. Volka Gowele (mwenye barakoa), Afisa wa Ubalozi.

Mafunzo hayo yameanzishwa kwa makubaliano kati ya Ubalozi na kampuni zote zinazoajiri wafanyakazi kutoka Tanzania ambao Ubalozi huwapatia barua kwa ajili ya kuthibitisha uhalali wao ili kupata kibali cha kuingia nchini humo. 

Mafunzo hayo ambayo hutolewa mara tu wanapowasili nchini humo, yanalenga kuwajengea uwezo wa kazi pamoja na kuwaelewesha sheria na taratibu za ajira za Qatar pamoja na haki zao za msingi. 

Pia mafunzo hayo yameanzishwa ili kuwajulisha maadili, mila na utamaduni za Qatar pamoja na kuwahimiza kujua wajibu wao ili kudumisha heshima ya Tanzania kimataifa na kuitangaza vyema nchi. 

Mafunzo ya awali yametolewa Desemba 12, 2020 kwa mabinti tisa kutoka Tanzania ambao wameajiriwa na Kampuni ya Qatar Manpower Solutions (WISA) inayomilikiwa na Serikali kwa ajili kufanya usafi na huduma za ndani. 

Mafunzo hayo ambayo yamesimamiwa na Bw. Volka Gowele, Afisa wa Ubalozi yameendeshwa na Bw. Sahim Ayoub Khatib, Diaspora wa Tanzania na mwajiriwa kwenye Kampuni ya HBK ya Qatar kwenye Kitengo cha Utawala na Rasilimali Watu. Bwana Khatib amejitolea kusaidia kuendesha mafunzo hayo kwa Watanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news