Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini (TFRA) inaendesha Mfumo wa Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja (Bulk Procurement System) kutoka nje ya nchi, mfumo ambao umejikita kupunguza bei na kuhamasisha matumizi ya mbolea kwa wakulima nchini.
Dhamira ikiwa ni ile ile ya kuhakikisha kuwa, wakulima nchini wanazalisha kwa tija na kwa manufaa zaidi ili waweze kujitosheleza kwa mahitaji ya chakula kwao binafsi, mahitaji ya Taifa na hata kuyauza nje kwa ajili ya kujiongezea vipato vitakavyowezesha kuimarisha uchumi.
Tazama maelezo ya makala hii fupi kutoka kwa kiongozi wa NFRA hapo juu ili uweze kupata picha kamili.