Hatimaye viongozi wa Umoja wa Ulaya wamefikia makubaliano yenye malengo makubwa ya kupunguza viwango vya gesi chafu kwa asilimia 55.
Wachambuzi wa masuala ya mazingira wamemweleza Mwandishi Diramakini kuwa, hiyo ni hatua kubwa ikilinganishwa na viwango vya mwaka1990, hali ambayo itaepusha kikwazo kikubwa kabla ya mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa hivi karibuni.

Uamuzi huo umefikiwa, baada ya mazungumzo ya usiku mzima wakati wa kikao chao cha siku mbili mjini Brussells,Ubelgiji ambapo nchi wanachama 27 za umoja huo zimeidhinisha pendekezo la Tume ya Utendaji ya Umoja wa Ulaya.
Pendekezo hilo linazingatia lengo mbadala la umoja huo kwa kufikia viwango vya hewa safi ifikapo nusu karne ili kuifanya Dunia kuwa mahali salama kwa ajili ya bianadamu kuishi.