URA SACCOS yashauriwa kufungua milango kwa watumishi wengine

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramdahani Kailima amewashauri viongozi wa Chama cha Ushirika wa Kuweka na Kukopa cha Jeshi la Polisi Tanzania (URA SACOSS) kufungua milango kuwaruhusu watu ambao sio watumishi wa jeshi hilo kujiunga na chama hicho cha kuweka na kukopa, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima akizungumza wakati akifungua mkutano mkuu wa 12 wa Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS) uliofanyika mjini
Tanga na kudhuhuriwa na viongozi wa matawi ya chama hicho kutoka nchi nzima.

Ushauri huo umetolewa na Kailima wakati akifungua mkutano mkuu wa 12 wa chama hicho uliofanyika mjini Tanga na kudhuhuriwa viongozi wa matawi ya chama hicho kutoka nchi nzima. 

Amesema kwamba, alikwishaoa ombi hilo mara kwa mara mpaka sasa hajaona mwekeleo wake na ndio maana ameona kutumia fursa hiyo kumuomba mwenyekiti mpya wa wa ushirika huo kuona namna ya kulifikiria suala hilo. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Ura Saccos, Benedict Wakulyamba akizungumza wakati wa mkutano huo.

“Mwenyekiti mpya naomba mje na mtazamo mpya kutumia kuwashawisha wajumbe kutoa fursa ya kuingia kwa watu ambao sio watumishi wa Jeshi la Polisi nao waweze kujiunga na Saccos hiyo,”amesema.  

Pia amewashauri waone namna ya kuweka vitega uchumi vitakavyowezesha Ura Saccos kuimairisha mtaji wake utawakowezesha kuongeza hisa na akiba na hatimaye kuwezesha kupunguza riba za wanachama na kuongeza kiwango cha kukopa hatimaye kukuza uchumi wa wanachama. 

“Ndugu zangu wanachama nimepitia ajenda za mkutano huo, hivyo kupitia fursa hii niwaombe muwe makini wakati mkipitia na kujadili mambo yanayowasilihwa kwa lengo la kuweka mikakati ya kuboresha ushirika wenu,”amesema. 
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, David Misime akizungumza wakati wa mkutano huo.

Naibu Katibu Mkuu huyo amewaasa viongozi Ura sacoss kufanya kila wanaloweza wawe muunganiko kati ya mafaniko ya URA SacCos na ustawi wanachama wa URA Sacoss. 

“Kama hatutakuwa na muunganiko kati ya mafanikio ya bilioni 73 mafanikio ya mwanachama mmoja mmoja itafikia kipindi wanachama watakata tamaa na kuona chama hakina faida,"amesema. 
Katika hatua nyingine, Naibu Katibu Mkuu huyo amegusia suala la rushwa ambapo amesema suala la rushwa wamekuwa wakilaumiwa nalo kwa kubambikia watu kesi. 

“Tunatumia kushawishi au kushiriki au kuomba niwaambie watumishi wenzangu hata vitabu vya dini vinaeleza rushwa ni mbaya hata kwa ustawi wenu na familia pia, kwani unaweza kupata kizazi cha ajabu ukashangaa kimetoka wapi,"amesema. 
Sehemu ya washirki kwenye mkutano huo wakifuatilia taarifa mbalimbali kwenye makabrasha yao.
Sehemu ya washirki kwenye mkutano huo wakifuatilia taarifa mbalimbali kwenye makabrasha yao.

“Maana asubuhi unaweza kuchukua rushwa ya mtu ambaye hali yake ni mbaya na umekwenda kununua unga umepeleka nyumbani usiku iwe ni askari wa kike au wa kiume umekula umeshiba halafu usiku mnatafuta mtoto kwa nguvu ya rushwa na atakayeingia tumboni ataaingia kwa nguvu ya rushwa,"amesema. 

Awali akizungumza wakati wa mkutano huo kabla ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu,Mwenyekiti wa Bodi ya Ura Saccos, Benedict Wakulyamba amesema ushirika huo wa ulianzishwa mwaka 2006 kwa madhumuni makubwa matano ikiwemo kujenga tabia miongoni mwa wanachama ya kujiwekea fedha za akiba. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramdahani Kailima (aliyekaa katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufungua mkutano huo kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ura Sacoss, Benedict Wakulyamba.

Amesema, akiba hiyo wanaiweka kutokana na mishahara yao na mapato ya kila siku yanayotokana na shughuli halali ambazo wanakuwa wakizifanya wakiwa watumishi wa Jeshi la Polisi. 

Pia amesema, mkutano huo ni muhimu sana huku akieleza kwamba uanachama wa Sacoss unawasaidia askari kupunguza makali ya maisha kutokana na kuwa na uwezo wa kukopa na kuweka akiba. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news