Utabiri wa hali ya hewa wa saa 24 zijazo kuanzia saa 3 usiku leo Desemba 16, 2020 unaowasilishwa na mchambuzi Noel Mlay kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), mvua na ngurumo zinatarajiwa kuendelea katika mikoa inayozunguka Ziwa Victoria pamoja na Magharibi mwa nchi.