Vijana 36 wa Kitanzania wapata fursa ya mafunzo ya kilimo Israel

Zaidi ya vijana 36 waliohitimu elimu ya kilimo katika Chuo Kikuu cha Sokoine wanaondoka nchini kuelekea nchini Israel baada ya kupata fursa ya mafunzo ya kilimo yaliyoratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Wafanyakazi wakiendelea na shughuli za kilimo nchini Israel kama walivyokutwa hivi karibuni. Israel inaongozwa kwa mifumo bora ya kilimo cha kisasa. (Picha na Eliyahu Hershkovitz).

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge wakati akiwakabidhi vijana hao tiketi za ndege pamoja na hati za kusafiria Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu, Bw. Alex Mfungo amewataka vijana hao kuzingatia mafunzo watakayoyapata wawapo nchini Israel kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Mfungo amesema, kwa kufanya hivyo watasaidia kufanikisha jitihada za Serikali za kuleta mapinduzi katika sekta ya kilimo ambacho kinategemewa na Watanzania wengi na kukifanya kilimo kuwa biashara na ajira.                                            

ALEX MFUNGO LIVEBwana Mfungo pia amewaasa vjana hao 36 wa Kitanzania wanaokwenda Israel kwa mafunzo ya kilimo kuzingatia sheria na taratibu za nchi hiyo na kuepuka kuvunja sheria pamoja na kuzingatia jukumu kubwa la kuwa mabalozi wazuri kwa Tanzania jambo litakalowezesha kupata fursa zaidi kwa wanafunzi wa Kitanzania.

Mratibu wa safari hiyo ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Leonce Bilauri amesema maagizo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa mwaka 2020 hadi 2025 imeielekeza Serikali kuboresha na kuongeza fursa za kilimo.

Lengo likiwa ni  kupunguza tatizo la ajira kwa vijana ambapo kwa kuzingatia hilo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeanza utekelezaji huo kwa kuwatafutia wanafunzi hao nafasi ya kujifunza nchini Isarel. 

LEONCE BILAURI LIVE

Mmoja wa vijana waliopata fursa ya kwenda nchini Israel, Bw.William Msemo ameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutekeleza kwa vitendo fursa za kutoa elimu ya kilimo bora kwa vijana jambo litakalowafanya kupunguza tatizo kwa ajira kwa vijana na kuahidi kuisambaza elimu hiyo kwa vijana wengine pindi watakaporejea

Wanafunzi hao 36 ni awamu ya kwanza ya vijana wa Kitanzania wanaokwenda nchini Israel kwa mafunzo ya kilimo kwa kipindi cha mwaka mmoja na awamu nyingine itafuata hivi karibuni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news