Vijana watakiwa kujikita katika ujasiriamali

Vijana nchini wametakiwa kutokubali kukaa mitaani, badala yake wajishughulishe na shughuli za ujasiriamili ili kujikimu kimaendeleo na kuendelea kuilinda amani iliyopo nchini, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi, Shaaban Seif Mohamed ametoa kauli hiyo katika hafla maalum ya kuwakabidhi vifaa vya kutendea kazi vijana 14.

Vijana ambao ni miongoni mwa walionufaika na mradi wa kuwasaidia vijana, hafla iliyofanyika ukumbi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Vuga jijini Zanzibar.

Amesema, Serikali ya Awamu ya Nane chini ya uongozi wa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, imepanga mikakati madhubuti ya kuhakikisha vijana wanaondokana na tabia ya kukaa mitaani bila ya kujishuhghulisha na shughuli zozote za kujikimu kimaisha, kama ilivyoelezwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 – 2025, badala yake wajishughulishe na kuondokana na fikra ya kusubiri ajira serikalini. 

Katibu Shaaban amesema, ni wajibu wa vijana hao kuvitunza vifaa hivyo walivyokabidhiwa kwa kuthamini nguvu za serikali na UNDP, pamoja na mashirika mbali mbali ya kimaifa yenye kuunga mkono juhudi za serikali katika kuhakikisha vijana wanajikwamua na janga la ajira nchi.

Akizungungumzia suala la elimu, Katibu Shaaban amewataka vijana hao waliopata fursa hiyo, kuwa ni mfano kwa vijana wengine, na aliwasihi wawe mabalozi kwa wenzao katika kueleza azma njema ya serikali ya awamu ya nane katika kutatua changamoto ya ajira hasa kwa vijana, kama ilivyoelezwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uratibu wa Shughuli za Serikali,Khalid Bakari Amran amesema Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa kuwa ndio wasimamizi wakuu wa watekelezaji wa ilani ni jukumu la Wizara kusimamia suala la kuwawezesha vijana kuweza kupata fursa mbalimbali ili kuwasaidia kuweza kujikimu kimaisha.  

Aidha, amelishukuru Shirikila la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa kulifikiria rika la vijana kwa kuwaletea mradi huo ili kuweza kuwasaidia katika kupambana na suala la ukosefu wa ajira nchini.

Kwa upande wake mratibu kutoka UNDP,Ali Shaibu amesema UNDP imeonelea kuwasaidia vijana katika suala la ajira, kwa kuwa tatizo hilo huwapelekea vijana kujihusisha na matendo maovu na hatarishi amabyo kupelekea kuharibika kwa jamii. Aidha amesema mradi huu umewasaidia vijana saba hadi sasa wanaendelea na mradi wa ufigaji kuku.

Jumla ya vijana 14 wamepatiwa vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 15, na kupatiwa vyeti vya kumaliza masomo ya ujasiriamali. Katika mradi unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi chini ya usimamizi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news