Waziri Biteko afuta leseni sita za wafanyabiashara wa madini

Waziri wa Madini, Doto Biteko amefuta leseni sita za wafanyabiashara wa madini ya dhahabu ambao wanatuhumiwa kujishughulisha na utoroshaji wa madini wilayani Chunya Mkoa wa Mbeya. Watuhumiwa hao wametakiwa kutojishughulisha na shughuli yoyote ya madini nchini, anaripoti Tito Mselem (WM) Chunya.

Wakati huo huo, Waziri Biteko ameagiza kuondolewa kwa Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Madini ya dhahabu anayehusika na usimamizi wa Soko la Madini la Chunya, Gagala Poul.
Vile vile Waziri Biteko amewasimamisha kazi watumishi watatu wa Ofisi ya Madini wa Mkoa wa kimadini wa Chunya baada ya kutuhumiwa kushirikiana na wafanyabiashara kutorosha madini, ambao watumishi hao ni Gabliel Masai, Edward Gavana na George Wandiga.

Pia, Waziri Biteko, ameagiza kusajiliwa kwa mialo yate inayochenjua madini ya dhahabu wilayani Chunya ili kujua mwalo gani umezalisha kiasi gani cha dhahabu na dhahabu hiyo imepelekwa kuuzwa soko gani.
“Bora tubaki na wanunuzi wawili wa madini ya dhahabu ambao ni waanifu kuliko kuwa na mlolongo wa wanunuzi ambao sio waaminifu na wasiofuata kanuni, taratibu na sheria zilizowekwa,”amesema Waziri Biteko.

Waziri Biteko amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila kutoa zawadi kwa wale wote watakaosaidia kupatikana kwa watu wanaotorosha madini.

“Niwaombe wachimbaji na wafanyabiashara wote wa madini kutoa ushirikiano kwa Serikali ili kukomesha tatizo la utoroshaji madini, tunataka nidhamu kwenye sekta ya madini ili tulete tija na maendeleo nchini,”amesema Waziri Biteko. 

Pia Waziri Biteko, amewataka wachimbaji na wafanyabiashara wote wa madini nchini kuhakikisha wanapeleka madini yao sokoni na kuachana na ufanyaji biashara ya madini nje ya masoko ya madini.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amempongoza Waziri wa Madini kwa kuchaguliwa kuwa mbunge wa Bukombe na kuteuliwa tena kuwa Waziri wa Madini.

Pia, Chalamila amesema tayari Serikali imeanza kujenga gereza ili watu watakaokamatwa wakitorosha madini hawatapekwa Mbeya Mjini bali watafungwa katika gereza hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news