Waziri wa Madini, Doto Biteko, leo Desemba 14, 2020, amemvua madaraka Mwenyekiti wa Soko la Madini Chunya, Gagala Poul pamoja na kuwasimamisha kazi watumishi wengine watatu,anaripoti Mwandishi Diramakini.
Watumishi hao watatu wa Ofisi ya Madini wa Mkoa wa kimadini wa Chunya wamesimamishwa baada ya kutuhumiwa kushirikiana na wafanyabiashara kutorosha madini, ambao ni Gabliel Masai, Edward Gavana na George Wandiga.Biteko amefanya maamuzi hayo leo alipotembelea soko hilo katika ziara yake anayoendelea nayo, ikiwa ni siku chache tangu ateuliwe na kuapishwa kuitumikia Wizara hiyo, ambapo amesema Mwenyekiti huyo amekuwa na uzembe kiasi cha madini kutoroshwa.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amemwagiza RPC kuwakamata wahusika wote na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria mara moja.
Tags
Uchumi