Waziri Chamuriho: Acheni kufanya kazi kwa mazoea

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Dkt. Leonard Chamuriho amewataka watumishi wa Wizara Ujenzi na Uchukuzi kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi ili kuongeza ufanisi, anaripoti Mwandishi Diramakini (Dodoma).

Akizungumza na menejimenti ya Sekta ya Ujenzi na Uchukuzi mara baada ya kuwasili ofisini leo jijini Dodoma ameitaka menejimneti kuunganisha wafanyakazi wa sekta zote kufanya kazi kwa kuzingatia matokeo yanayopimika.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho, akisisitiza jambo kwa menejimenti ya wizara hiyo, mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za wizara jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, Kulia ni Katibu Mkuu-Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga.
Kaimu Katibu Mkuu-Uchukuzi, Gabriel Migire akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho na Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, mara baada ya kuwasili ofisini hapo kuanza kazi jijini Dodoma leo. 

“Jipangeni kuhakikisha kuwa Watumishi wote wanafanya kazi kwa umoja na ushirikiano ili kufikia malengo yanayotarajiwa na Serikali katika kuboresha miundombinu nchini,”amesema Mhandisi Dkt. Chamuriho.

Amemtaka Katibu Mkuu-Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga na Kaimu Katibu Mkuu Uchukuzi, Gabriel Migire kuhakikisha miradi yote inayoendelea ujenzi wake unakamilika kwa wakati na tija.
Katibu Mkuu-Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga akiwakaribisha wizarani Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho na Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya mara baada ya kuwasili ofisini hapo kuanza kazi jijini Dodoma leo.
Naibu Waziri Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akisisitiza jambo kwa menejimenti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za wizara jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho kulia ni Katibu Mkuu-Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga na kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Uchukuzi Gabriel Migire.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi,Mhandisi Godfrey Kasekenya ameitaka menejimenti ya wizara kuweka ratiba ya mara kwa mara ya kukagua miradi ili kupata taarifa ya maendeleo na kuchukua hatua mapema kwa miradi yenye changamoto. 

Akiwakaribisha Waziri na Naibu Waziri, Katibu Mkuu Ujenzi amewahakikishia viongozi hao ushirikiano kati yao menejimenti na watumishi kwa sekta anazosimamia.

Waziri Mhandisi. Dkt. Leonard Chamuriho na Naibu Waziri Eng. Godfrey Kasekenya walikuwa katika kikao cha kwanza cha na menejimenti ya wizara mara baada ya kuteueliwa kuongoza wizara hiyo hivi karibini.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho, katika picha ya Pamoja na menejimenti ya Wizara hiyo, mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news