Waziri Jafo aagiza wakurugenzi wanne Halmashauri kuchukuliwa hatua

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (OR-TAMISEMI), Mhe.Selemani Jafo amemwagiza Katibu Mkuu, Joseph Nyamhanga kuwachukulia hatua wakurugenzi wa halmashauri nne, walioshindwa kutoa ruhusa kwa wakuu wa shule za sekondari kuhudhuria mkutano wao mkuu wa mwaka, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Mhe.Jafo ametoa maagizo hayo leo Desemba 21,2020 wakati alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania Bara (TAHOSSA) unaofanyika jijini Dodoma.

Waziri Jafo amewataja wakurugenzi hao kuwa ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Wilaya ya Kahama, Korogwe na Sikonge.

“Mkutano kama huu ndiyo sehemu ambayo Serikali inatumia kutoa maagizo kwa wakuu wa shule katika usimamizi wa masuala mbalimbali ya kielimu, lazima wahudhurie ili wapate maagizo hayo. Serikali ya awamu ya tano imetoa fedha nyingi katika kuboresha miundombinu ya elimu ambayo wasimamizi wakuu ni wakuu wa shule za sekondari, hivyo ushiriki wao katika mkutano huo ni jambo la lazima,"amesema Waziri Jafo.
Amesema, uwepo wa wakuu hao wa shule na Serikali katika mkutano huo inapatikana fursa kutoa maagizo, huku Iakiwashangaa wakurugenzi walishindwa kutoa vibali kwa wakuu wa shule kuhudhuria katika mkutano huo.

Waziri Jafo ameagiza wakurugenzi wote wa halmashauri nchini kuhakikisha mwaka 2021, wanasimamia upimaji wa maeneo ya shule ili kupata hati miliki na kuondoa migogoro ya ardhi.

Amesema, ni aibu kwa Mkurugenzi kuwa na afisa ardhi katika ofisi yake, lakini maeneo mengi ya shule hayajapimwa, hali inayosabaisha uvamizi wa maeneo na migogoro ya ardhi baina ya taasisi na wananchi katika maeneo husika.

Amesema, katika mwaka wa fedha 2020/21 Serikali imetengaz zaidiya sh. bilioni 68 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 2,088.

Pia wametenga kiasi cha sh. bilioni 42.3 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya maabara ili kuwezesha vijana wanaosoma masomo ya sayansi kujifunza kwa vitendo.

Rais wa Chama cha Wakuu wa Shule Tanzania Bara (TAHOSSA),Vitaris Shija amesema mkutano huo ni wa 15 kufanyika na kuiomba Serikali kupima maeneo ya shule ili kuondokana na migogoro ya ardhi.

Katibu Mtendaji wa NACTE, Dkt.Adolf Rutayuga amesema wameshiriki katika mkutano huo kutokana wateja wao wakuu kutoka katika shule za sekondari hivyo watakuwa na fursa ya kukutana na wakuu wa shule pamoja na wadau wengine wa elimu nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news