Waziri Jafo aipongeza Kilwa kwa ujenzi wa kituo bora cha afya Somanga

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo (Mb) ametoa pongezi kwa viongozi na watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kwa usimamizi mzuri wa fedha ziilizotolewa kujenga Kituo cha Afya Somanga, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Mheshimiwa Jaffo alisema hayo leo Disemba 14, 2020 kwenye ziara yake Mkoani Lindi, ambapo alianza kwa kutembelea kituo cha Afya Somanga kukagua maendeleo ya ujenzi.
“Ndugu zangu leo nipo katika ziara yangu Mkoa wa Lindi, na nimeamua kuanzia hapa kwa sababu Mhe. Rais Katika ziara zake, alipopita hapa wananchi walimwambia shida yao kubwa ni kituo cha Afya. Mheshimiwa Rais kwa upendo wake wa dhati kwa wananchi wa Kilwa, akatoa milioni 20 kama mchango wake,"amesema Jafo.

Pia Mheshimiwa Jafo amesema kuwa ,ameridhishwa sana kuona kuwa fedha ziilizotolewa na Mheshimiwa RaisiJohn Pombe Magufuli zimeenda kwenye mikono salama na zimetendewa haki.

Aidha alieleza kuwa kituo hicho kimejengwa vizuri sana na Kitakuwa ni miongoni mwa vituo bora vya Afya vyakupigiwa mfano hapa Nchini vitakavyofunguliwa karibuni.

“ Binafsi nikiwa kama msaidizi wa karibu wa Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli, nimeridhika sana na kazi kubwa iliyofanyika hapa na nitahakikisha tunapata vifaa kwa haraka ili sasa wananchi wapate huduma bora,"amesema Jafo.

Kwa upande mwingine Ndugu Shewaji Kimbwembwe maarufu kama Mzee wa Jogoo ( aliyempa Rais zawadi ya Jogoo ), akiongea kwa niaba ya wananchi wa Somanga amesema:
“Tunamshukuru sana Rais John Pombe Magufuli kwa utendaji wake katika maeneo yote. Kituo hiki cha Afya kimethibitisha upendo wake wa dhati kwetu sisi wananchi. Tunachokiomba tu sasa Vifaa vije haraka ili tufaidike na neema hii hapa Somanga,"amesema Kimbwembwe.

Awali mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi, alimueleza Waziri Jafo juu ya upungufu wa watumishi wa Afya katika Mkoa wa Lindi na kumuomba kufanya jitihada za dhati ili wapate watumishi watakaokidhi mahitaji. Pia aliomba OR-TAMISEMI kusaidia katika kuiboresha Hospitali ya Wilaya ya Lindi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news