Waziri Lukuvi apokea ripoti mgogoro wa ardhi Chang'ombe

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi amekutana na kamati maalum iliyokuwa inashughulikia mgogoro wa matumizi ya ardhi Kata ya Chang’ombe jijini Dodoma leo Desemba 11,2020 ambapo amepokea taarifa kuhusu mgogoro huo,anaripoti Eliafile Solla (WANMM).Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akifuatilia uwasilishaji wa taarifa ya kushughulikia mgogoro wa matumizi ya ardhi uliodumu kwa muda mrefu katika Kata ya Mtakuja, Mtaa wa Chang’ombe jijini Dodoma.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi (wa kwanza kushoto) akifuatilia taarifa ya kushughulikia mgogoro wa matumizi ya ardhi uliodumu kwa muda mrefu katika Kata ya Mtakuja, Mtaa wa Chang’ombe jijini Dodoma iliyowasilishwa kwake na kamati maalum iliyoundwa na Serikali.

Mgogoro wa matumizi ya ardhi wa Mtakuja, Kata ya Chang’ombe katika eneo lenye hekta 10 umedumu kwa muda mrefu licha ya jitihada mbalimbali za Serikali za kuutafutia ufumbuzi.

Serikali iliunda kamati maalum ya kushughulikia mgogoro huo wa matumizi ya ardhi na baadae kuamua kupanga na kupima eneo hilo na kubadilisha matumizi kutoka yale ya awali na kuwa makazi kutokana na uhalisia na maendelezo yaliyokwisha kufanyika kupitia mradi wa maboresho wa mwaka 2015.
Mjumbe kutoka kamati maalum ya kushughulia mgogoro wa Mtakuja Ndugu Wincheslaus Kweyunga (aliyesimama) akiwasilisha taarifa ya kushughulikia mgogoro wa Mtakuja kwa Mhe. Lukuvi Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Mjumbe kutoka kamati ya kushughulia mgogoro wa Mtakuja Ndugu Wincheslaus Kweyunga (aliyesimama) akiwasilisha taarifa ya kushughulikia mgogoro wa Mtakuja kwa Mhe. Lukuvi Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Kamati hiyo imekutana na Mhe. Lukuvi jijini Dodoma leo na kuwasilisha taarifa na mapendekezo yake jinsi ya kuushughulikia mgogoro huo ambapo Mhe. Waziri Lukuvi atatoa maagizo baada ya kuipitia taarifa hiyo na kujiridhisha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news