Waziri Mkuchika atoa maagizo kwa watumishi wote

Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja taasisi zake wametakiwa kuitekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya Mwaka 2020-2025 katika eneo la Utumishi wa Umma na Utawala Bora ili wananchi wanufaike na huduma zitolewazo na ofisi hiyo,anaripoti James K. Mwanamyoto (OR-UTUMISHI) Dodoma. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George akizungumza na watumishi wa ofisi yake mara baada ya kuripoti rasmi leo. Kushoto kwake ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi. Na kulia kwake ni Katibu Mkuu – UTUMISHI, Dkt. Laurean Ndumbaro. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Ofisi yake Jijini Dodoma mara baada ya kuripoti rasmi leo. Kulia kwake ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi na Katibu Mkuu-UTUMISHI, Dkt. Laurean Ndumbaro na Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Francis Michael. 

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika mara baada ya kupokelewa na Watumishi wa Ofisi yake jijini Dodoma ikiwa ni siku chache tangu ateuliwe na kuapishwa rasmi na Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. 

Mhe. Mkuchika amesema Ofisi yake na taasisi zote zilizo chini ya Ofisi yake ambazo ni TAKUKURU, MKURABITA, TASAF, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Chuo cha Utumishi wa Umma, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na Wakala ya Ndege za Serikali zinatakiwa zikae na kuandaa mpango madhubuti wa miaka mitano ili kutekeleza ahadi za masuala ya kiutumishi na Utawala Bora zilizoainishwa katika Ilani ya CCM. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na watumishi wa ofisi yake (hawapo pichani) mara baada ya kuripoti rasmi leo na kuanza kazi. 

“Watumishi wa Umma tunapaswa kuitumikia Serikali iliyoshinda uchaguzi ambayo ni ya CCM na CCM inayo Ilani iliyoiweka Serikali madarakani, hivyo hatuna budi kuitekeleza,” Mhe. Mkuchika amesisitiza. 

Aidha, Mhe. Mkuchika ametoa rai kwa watumishi kuendelea kutoa ushirikiano katika kipindi hiki alichokabidhiwa tena jukumu la kusimamia utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo. 

Kwa upande wake, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amemuahidi Mhe. Mkuchika na Watumishi ushirikiano katika kuwatumikia Watanzania kama ambayo Mhe. Rais Magufuli anatarajia. 
Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George mara baada ya kiongozi huyo kuripoti rasmi ofisini kwake leo jijini Dodoma. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George akisalimiana na baadhi ya Wakurugenzi wa ofisi yake mara baada ya kuripoti rasmi leo 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika akimkabidhi nyaraka za kiutumishi Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi mara baada ya Viongozi hao kuripoti rasmi leo ofisini na kuanza kazi. 

Sanjari na hilo, Mhe. Ndejembi ameomba ushirikiano kutoka kwa Watumishi na Menejimenti kwa ujumla ili kuhakikisha huduma bora inatolewa kwa wananchi. 

Mhe. Mkuchika na Mhe. Ndejembi wamepokelewa leo na Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora tayari kwa kuanza kazi rasmi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news