Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa amlilia Subash Patel

Waziri Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Edward Lowassa ameelezea kushtushwa kwake na kifo cha mfanyabiashara maarufu nchini Subash Patel, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi yake imesema, Lowassa ambaye mwaka 2015 alikuwa mgombea urais kwa tiketi ya upinzani kabla ya kurejea CCM, amestushwa sana na msiba huo.

"Nimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo cha rafiki na mzalendo halisi wa nchi hii Subash Patel.
Nimefahamiana na Subash kwa muda mrefu na ukaribu wangu na yeye ulitokana na moyo wake wa kulisaidia taifa hili na watu wake.

“Wakati nikiwa na majukumu serikalini nilishuhudia jinsi alivyosaidia miradi mingi vijijini, yenye nia ya kuwatoa watanzania kwenye umasikini.Hakika taifa limempoteza mmoja wa wazalendo halisi.Natoa pole kwa familia pamoja na Watanzania kwa kifo cha Subash. Om Shamti! Om Shamti,"amesema Waziri Mkuu mstaafu mzee Lowassa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news