Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango, Jamal Kassim Ali amemuagiza Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Ofisi ya Zanzibar kuwasimamisha kazi watendaji watakaobainika kuingiza mzigo kwa bei ndogo ili kupisha kufanyika uchunguzi, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Akizungumza katika ziara ya kuangalia utendaji wa Bandari na Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume akiambatana na Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi, Rahma Kassim Ali amesema Serikali haijaridhika na mfumo wa ukusanyaji wa mapato na kuwataka kuiboresha mifumo hiyo ili kuweza kutoa huduma bora zaidi.

Amesema katika ziara hiyo bandarini wamebaini mzigo ulioingizwa kwa bei ndogo kinyume na utaratibu jambo linaloashiria utendaji usioridhisha na viashiria vya kuvuja mapato na kuitia hasara Serikali.
Aidha, ameitaka mamlaka ya viwanja vya ndege Zanzibar kujiandaa kwa kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wao ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi wakati itakapofika Desemba 31, mwaka huu ambapo watakabidhiwa kiwanja hicho cha Terminal 3 ili kuweza kuleta tija kwa watumiaji na Taifa kwa ujumla.
Nae Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Rahma Kasim Ali amewakumbusha wafanyabiashara kulipa kodi ili kuiwezesha Serikali kujiendesha kwa kutatua matatizo ya wananchi ikiwemo elimu,afya na barabara.

Tags
Zanzibar