Wizara ya Madini imedhamiria kuendeleza mageuzi makubwa katika sekta hiyo ili kuyafikia matokeo chanya kwa haraka, hatua ambayo itawezesha kuimarisha uchumi nchini kupitia rasilimali hizo, anaripoti Mwandishi Diramakini.
"Tufurahie tujikua na kukumbuka tuna kazi kubwa mbele yetu za kufanya, kinachotakiwa kwetu kwa sasa ni matokeo, kama mnavyofahamu umuhimu wa sekta yetu kwa maendeleo ya nchi. Nyumba yetu inafuraha sana, tumepata kiongozi ambaye ametoka miongoni mwetu, namshukuru sana Mungu kwa ajili yako, kama familia ya madini tunakupongeza sana.
"Ukiona Mheshimiwa Rais ambaye ana watu zaidi ya milioni 50 amekuchagua, ni kwa sababu ya matokeo mazuri yaliyoonekana kwenye sekta ya Madini. Mafanikio haya si ya Manya ni kwenu nyote, nawapongeza sana kwa ushirikiano mliompatia ikapelekea kupata nafasi.
"Uchimbaji wa makaa ya mawe lazima uanze,"Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyasema hayo leo Desemba 11, 2020 wakati wakimpokea Naibu Waziri wa Madini, Prof.Shukrani Manya baada ya kuteuliwa na kuapishwa leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Madini, Prof. Shukrani Manya amesema kuwa, "sisemi kwamba ni kwa sababu ya uelewa, vipaji, talanta wala maarifa bali wizara na taasisi zake hususan Tume ya Madini. Matokeo yenu mazuri yamenipa ngazi ya kupandia, yaliyofanyika kwenye Sekta ya Madini yanaonekana.
"Mheshimiwa Rais anatamani Sekta ya Madini kutoka hatua moja kwenda nyingine, tuendelee kufanyiakazi maono yake ili tujenge uchumi wa nchi yetu. "Nashukuru nipo kwenye jamii ya watu ninaowafahamu, nawashukuru sana kwa ushirikiano mlionipatia kwa kipindi cha miaka mitatu ambayo tumefanya kazi pamoja, tuendelee kushirikiana ili Sekta ya Madini iendelee.
"Ninaamini nitaendelea kuwa bora ili kuwa kiongozi niitumikie nafasi hii. Ubunge ni kitu ambacho sikuwahi kukiwaza, ninaamini kwa pamoja tutavuka.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila amesema,watapeana ushirikiano mkubwa ili kuhakikisha Sekta ya Madini inaleta matokeo makubwa zaidi nchini.
"Amekuja mwenzetu, tunajuana, kama ni madaraka atajifunza, tunaahidi kuendelea kushirikiana ili kuyatekeleza kwa vitendo maono ya Mheshimiwa Rais Dkt.John Pombe Joseph Magufuli ya kuifanya sekta hii kuwa na mchango mkubwa katika uchumi wetu,"amesema.