12 wakamatwa wakijaza ajira feki za Idara Maalum

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Serikali wamefanikiwa kuwakamata watu 12 wanaodhaniwa ni wahalifu wakiwa wanaendesha zoezi haramu la upigaji picha na ujazaji mikataba inayosadikiwa ya ajira, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Akizungumza mara baada ya kuendeshwa kwa opereshi hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ, Mhe. Masoud Ali Mohammed amesema zoezi hilo wamebaini kuwa zoezi hilo limekua likiendeshwa katika nyumba ya mtu binafsi ambapo linatajwa kuwa na nia ovu lenye kusadikiwa na ujazaji wa mikataba ya ajira katika Idara Maalum.

Kwa upande wake Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kusini Unguja, ACP Kombo Khamis Kombo amesema taarifa hizo wamezipata kutoka kwa raia wema na wamefanikiwa kuwakamata watu 12 ambapo amesema wanaendelea kuchunguza zaidi ili kubaini wahusika na kiini juu ya tukio hilo.

Kamanda Kombo amesema licha ya kuwakamata watu hao pia wamekamata sare zinazofananishwa na kikosi cha Kujenga Uchumi JKU,kompyuta mpakato,kamera pamoja na gari na vyombo vya maringi mawili.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Mhe Hadidi Rashid amehakikisha kuwa wale wote waliohusika pamoja na mmiliki wa nyumba hiyo wanakamatwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

  1. HONGERA MH.WAZIRI KWA KAZI NZURI, PIA NITOE WITO KWA JAMII KUTOWAFUMBIA MACHO WATU KAMA HAO KWANI BADO WAPO WENGI HUTOA AJIRA ZA VIKOSI KINYEMELA NA KITAPELI RAIA.

    ReplyDelete
Previous Post Next Post

International news