Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) limesema kuwa, aina mpya ya virusi vya Corona vinavyosambaa kwa kasi kuliko aina ya kwanza imegunduliwa katika nchini za Botswana, Zambia, Gambia na Kenya.
Mkurugenzi wa shirika hilo barani Afrika, Matshidiso Moeti amesema kwamba, virusi hivyo vinasambaa kwa kasi kutokana na safari nyingi za watu kote barani Afrika.
Katika kikao na waandishi wa habari, Matshidiso amesema kwamba, mpango wa COVAX, wa shirika hilo unaolenga kutoa chanjo kwa nchi maskini, unapanga kutoa dozi milioni 600 dhidi ya virusi vya Corona kote Afrika ndani ya mwaka huu.
Amesema kwamba, watu milioni 3.3 wameambukizwa virusi vya Corona kote Afrika hadi sasa.