Arsene Wenger atamani kurejea Arsenal kuokoa jahazi

Mzee Arsene Wenger (71) amesema yupo tayari kurejea uwanjani Emirates kumsaidia kocha Mikel Arteta kurejeshea wababe hao katika reli iwapo uongozi wa klabu ya Arsenal utamuhitaji, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Kocha wa zamani wa Arsenal, mzee Arsene Wenger. (Picha na Getty Images/ Diramakini) 

Pia amesema, wapo Arsenal watazama tena jinsi hali ilivyokuwa katika mechi saba za awali kabla ya kocha Arteta kuongoza kikosi hicho dhidi ya Chelsea kwa ushindi wa 3-1 Desemba 26, 2020, yeye bila kinyongo yupo tayari kufanya jambo jipya. 

Aidha, tangu wakati huo, klabu ya Arsenal wamesajili ushindi wa 1-0 dhidi ya Brighton na mwingine wa 4-0 dhidi ya West Bromwich Albion. 

Wachambuzi wa soka wamemueleza Mwandishi Diramakini kuwa, mwanzo mbaya katika kampeni za Ligi Kuu ya England (EPL) msimu huu chini ya kocha Arteta aliyepewa kandarasi Desemba, 2019 umewadhoofisha Arsenal ambao wanashikilia nafasi ya 11 kwa alama 23 baada ya mechi 17 hadi sasa. 

Mzee Wenger alihudumu katika mafunzo kwa Arsenal kwa miaka 22 kabla ya kuagana na kikosi hicho mwishoni mwa msimu wa 2017-18. 

“Iwapo nitahitajika, nitarudi ili nimsaidie Arteta kufanya kazi. Japo sitarajii hilo kufanyika kwa sasa kwa sababu kikosi kimeanza kujitutumua. Lakini kikiyumba tena na nione dalili za kuzama kwa jahazi, nitafanya hima na kwenda kuokoa bila ya kusubiri kuambiwa,”amekaririwa Kocha huyo Mzee.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news