Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Mheshimiwa Wang Yi amesema kuwa, Taifa lake limedhamiria kustawisha uhusiano na nchi za Afrika katika nyanja mbalimbali ikiwemo kidplomasia, kiuchumi na mambo mengine, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi. (Picha na Thomas Trutschel/Photothek via Getty Images/ Diramakini).
Yi ameyabainisha hayo katika mahojiano mahojiano mahojiano maalum na shirika la habari la nchi hiyo la Xinhua mjini Beijing.
Amesema, uhusiano wa China na Afrika umepanuka zaidi hususani katika kipindi hiki cha kupambana na janga la virusi vya corona (COVID-19), kwani licha ya wao kukabiliana na janga hilo, pia wamekuwa mstari wa mbele kuwezesha juhudi za kuukabili ugonjwa huo barani Afrika.
Kwa mujibu wa Waziri Yi, Jamhuri ya Watu wa China ni miongoni mwa mataifa makubwa duniani ambayo yanaendelea kustawi kwa kasi zaidi, hivyo mafanikio yao wanaamini pia yanapaswa kuwa na mchango wa kustawisha Afrika katika nyanja mbalimbali.
Wachambuzi wa masuala ya kiuchumi wanaitaja China kama mshirika mkubwa wa maendeleo barani Afrika ambaye amechangia kwa kiwango kikubwa ustawi wa miradi mbalimbali ikiwemo miundombinu, nishati na mingineyo.