Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2020 na kuzitaja shule 10 zilizofanya vizuri, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Hayo ni kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (Nacte) Dkt. Charles E. Msonde wakati akitangaza matokeo ya darasa la nne, kidato cha pili na kidato cha nne mwaka 2020/2021 jijini Dar es Salaam.
Aidha, kupitia matokeo hayo Shule ya Wasichana ya St Francis ya mkoani Mbeya imeshika nafasi ya kwanza kitaifa.
Shule ya St. Francis imepanda kutoka nafasi ya pili iliyoshika mwaka juzi na kuishusha Shule ya Sekondari ya Kemebos ya mkoani Kagera hadi nafasi ya nne kwa sasa.
Dkt. Charles Msonde amezitaja shule nyingine tisa zilizofanya vizuri zaidi katika matokeo hayo kuwa ni Iliboru ya jijini Arusha, Cannosa ya jijini Dar es Salaam, Kemebos ya mkoani Kagera na Feza Boys ya jijini Dar es Salaam.
Amesema shule nyingine ni Ahmes, St. Aloysius Girls, Marian Boys mkoani Pwani na St. Augustine Tagaste ya jijini Dar es Salaam.
Tags
Habari