JKT yasitisha mafunzo kwa kundi la kujitolea 2020/2021

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limesitisha kwa muda mafunzo kwa kundi la kujitolea kwa mwaka 2020/2021 kwa vijana waliokuwa wamechaguliwa kushiriki mafunzo hayo yaliyotarajiwa kuanza hivi karibuni nchini kote, anaripoti Mwandishi Diramakini (Dodoma).
Kaimu Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Kanali Hassan Mabena akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kusitishwa kwa mafunzo ya kundi la kujitolea kwa mwaka 2020/2021 wakati wa mkutano uliofanyika makao makuu ya jeshi hilo wilayani Chamwino mkoani Dodoma leo Januari 19, 2021, Mafunzo hayo yalipangwa kuanza hivi karibuni katika makambi mbalimbali ya JKT.

Hayo yamesemwa leo na Kaimu Mkuu wa Utawala, Kanali Hassan Mabena wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo wilayani Chamwino mkoani Dodoma. 

“Kutokana na kusitishwa kwa mafunzo hayo, JKT inawataka vijana wote ambao walichaguliwa na kuripoti makambini kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa kujitolea warejee majumbani kwao,”amesisitiza Kanali Mabena. 

Pamoja na hayo, Kanali Mabena amewataka vijana ambao walikuwa hahawajaripoti wasiende kuripoti katika makambi waliyopangiwa mpaka watakapotangaziwa tena. 

Jeshi la Kujenga Taifa limekuwa likiwajengea vijana uwezo wa kujiajiri kupitia stadi za maisha wanazopata katika mafunzo yanayotolewa kwa mujibu wa sheria na yale ya vijana kujitolea, hivyo kuwawezesha kuwa wazalendo wanaoshiriki kikamilifu katika ujenzi wa Taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news