Jonas Mkude atozwa faini Milioni 2/-

Kamati ya Nidhamu ya Klabu ya Simba chini ya Mwenyekiti wake, Suleiman Kova imetangaza hukumu ya kiungo wa klabu hiyo, Jonas Mkude ambaye alisimamishwa na uongozi kwa makosa ya utovu wa nidhamu.
Kwa mujibu a Kova, haya ndiyo makosa matatu aliyokuwa akituhumiwa kuyafanya, pamoja na hukumu zake.

KOSA LA KWANZA: Kutohudhuria semina elekezi iliyohusisha wachezaji, benchi la ufundi na viongozi. Adhabu yake ni faini ya shilingi milioni moja (1,000,000).

KOSA LA PILI: Kuchelewa kuingia kambini wakati timu ilipokuwa ikijiandaa na mchezo dhidi ya Coastal Union. Adhabu aliyopewa ni karipio kali na faini ya shilingi milioni moja (1,000,000) pamoja na kuwekwa katika kipindi cha uangalizi cha miezi sita.

KOSA LA TATU: Kutoripoti kambini siku ya 26/12/2020 bila ruhusa. Katika tuhuma hizi, kamati haikumkuta na hatia baada ya kamati kutothibitisha pasipo shaka shitaka hilo.

MAAGIZO

Kamati imemtaka Mkude kurejea kambini mara moja kuendelea na mazoezi na asipofanya hivyo atakuwa amefanya tena kosa la utovu wa nidhamu.

Faini aliyotozwa anatakiwa kuilipa ndanI ya mwezi mmoja.

Kamati imemtaka Mkude kuomba radhi kwa maandishi ndani ya saa 24.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news