Waziri wa Mambo ya Nje na Mjumbe wa Baraza la Taifa wa China, Wang Yi akiwasili nchini leo Januari 7, 2021 kwa ziara ya siku mbili hadi
tarehe 8 mwezi huu 2021.
Ziara
hii ni matokeo ya mazungumzo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, John Magufuli aliyofanya kwa njia ya simu na Rais wa Chini Xi
Jinping Desemba 15, mwaka jana.
Katika ziara hii amepokelewa katika uwanja wa ndege wa Geita ulioko
wilayani Chato na atafungua na kuweka jiwe la msingi
katika Chuo cha Ufundi (Veta) wilayani Chato na kuzungumza na wananchi.
Waziri Wang Yi anafungua chuo hicho cha Veta cha Wilaya ya Chato kwa
sababu tatu ambazo kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Kabudi ni kumpa heshima kama mila zetu zilivyo
kwa mgeni anayekutembelea,pili ni kutambua kwamba nchi ya China imepiga
hatua kubwa katika teknolojia ya ufundi.
Ameongeza
kuwa, sababu ya tatu ni kutambua mchango wa nchi ya China ambayo kwa
sasa inajenga chuo cha Veta mkoani Kagera ambapo taifa hilo lilikubali
kujenga vyuo vya ufundi 50 kwa nchi za Afrika.
Profesa
Kabuni amefafanua kuwa, Waziri Wang Yi baada ya kufika Chato atafanya
mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli na
Baadaye atafanya mazungumzo na Waziri mwenzake wa Tanzania pamoja na
ujumbe wake.
Ameongeza
kuwa, siku ya pili Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi
atatembelea mwalo wa uvuvi wa samaki wa Chato katika ziwa Victoria ili
kujionea shughuli za uvuvi katika eneo hilo.
Tags
Habari