Maalim Seif apumzishwa baada ya kupata maambukizi ya Covid 19


Mwenyekiti wa ACT Taifa, Maalim Seif Sharif Hamad.
Chama cha ACT Wazalendo kinawajulisha wanachama wake, wanzanzibari, pamoja na umma wa Watanzania, kuwa Mwenyekiti wake wa Taifa, Maalim Seif Sharif Hamad, Mkewe, Bi Awena, pamoja na Wasaidizi wake kadhaa wa Karibu, wamethibitika kupata maambukizo ya Virusi vya Covid 19 baada ya kufanyiwa vipimo.

Katika hali ya kuchukua tahadhari zaidi Madaktari walimshauri Maalim Seif kuwa ni vyema awepo chini ya uangalizi maalum katika kipindi chote atakachokuwa anaendelea na matibabu dhidi ya Korona. Hivyo basi, tangu juzi Ijumaa jioni, Maalim Seif alipumzishwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Unguja, Zanzibar, ambako anaendelea kuwa chini ya uangalizi wa karibu wa Madaktari.

Tunapenda kuchukua nafasi hii kuujulisha umma kuwa hali ya Maalim Seif pamoja na Mkewe zinaendelea vyema kabisa, Viongozi wenzake pamoja na Wanafamilia wamekuwa na mawasiliano naye ya kawaida kila siku.

ACT Wazalendo tunawaomba wanachama wetu, wanzanzibari na watanzania wote kwa ujumla kumuombea dua Maalim Seif katika kipindi hiki ambacho amepumzishwa ili aweze kupona kwa haraka na arudi kuendelea na majukumu yake. Pia, tunarejea wito wetu kwa Watanzania wote kuchukua hatua za kujilinda dhidi ya ugonjwa

Ado Shaibu,

Katibu Mkuu,

ACT Wazalendo

31 Januari, 2021

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news