Mafuriko, maandamano, ajali ya ndege, volcano, utalii, mauzo

Picha iliyopigwa Januari 11, 2021 ikionyesha gari likiwa limezama katika maji ya mafuriko katikati ya barabara mjini Fushe Kosove baada ya mvua kubwa kunyesha Kosovo. (Picha na AFP/Diramakini).
Maafisa wa polisi wakiwa wanamdhibiti mmoja wa wanaharakati wa vijana nchini India wakati wa maandamano ya kupinga sheria mpya za kilimo mjini New Delhi, India siku ya Januari 12, 2021. (Picha na Reuters/Diramakini).
Maafisa wa Jeshi la Majini nchini Indonesia wakichukua picha za kiboksi cheusi  cha ndege ya Sriwijaya Air flight SJ 182, ambayo ilipata ajali Januari 12, 2021 katika Pwani ya Jakarta nchini humo. (Picha na Reuters/Diramakini). Afisa Usalama wa Jeshi la Marekani akiwa ameimarisha ulinzi mbele ya jengo la Bunge la Capitol wakati wakati wajumbe wa bunge hilo wakijiandaa kupiga kura ya kumtaka Makamu wa Rais Mike Pence na  Baraza la Mawaziri kumuondoa ofisini mjini Washington, Rais Donald Trump siku ya Januari 12, 2021 baada ya kukoa imani naye. (Picha na Reuters/ Diramakini).
Picha iliyochukuliwa kwa ndege isiyokuwa na rubani (drone) ikionyesha nyumba ziliyoharibiwa baada ya volcano ya Taal kulipuka mjini Batangas, Ufilipino siku ya Januari 12, 2021. (Picha na EPA-EFE/Diramakini).
Wapita njia wakionekana wakipita kwa tabu katika wingu nzito lililojaa barafu mjini Helsinki nchini Finland siku ya Januari 12, 2021. (Picha na Afp/Diramakini). Nyani wa Kijapan waliopigwa picha eneo la Hakodate Tropical Botanical Garden mjini Hakodate uliopo Kaskazini mwa Kisiwa cha Hokkaido ambao ni kivutio kikubwa cha utalii wakiwa wameweka pozi. Picha imepigwa na Kyodo siku ya Januari 12, 2021. (Picha na Kyondo/ Reuters/Diramakini). 
Mwanamke anayeendesha baiskeli huku akiuza maua ya kutengeneza katika barabara ya Long Bien karibu na daraja la Hanoi. (Picha na Afp/ Diramakini).  Watoto wakitumia boti kuvuka upande wa pili katika Kijiji cha Obot karibu na Shkodra, Albania baada ya mvua kubwa kunyesha Januari 12, 2021. (Picha na Reuters/ Diramakini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news