Makachero rasmi msako wa wakwepa kodi nchini

Makachero wa Jeshi la Polisi nchini kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na taasisi zingine za usimamizi wa sheria wanatarajia kuendesha operesheni ya pamoja nchi nzima dhidi ya wafanyabiashara ambao wamekuwa wakikwepa kulipa kodi, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Sambamba na wanaokaidi kutumia mashine za Kielektroniki za EFDs au wanunuzi ambao huwa hawadai risiti baada ya manunuzi.

Kamishina wa Polisi, Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu, CP Benedict Wakulyamba ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro jijini Dodoma.

Ameagiza makamanda wa polisi wote nchini pamoja na Zanzibar kuhakikisha wanakabiliana na wafanyabiashara hao wanaokwepa kodi.

Pia amesema, Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kwa wote wanaojihusisha na vitendo hivyo kuacha mara moja.

"Misako itaendeshwa kwenye maeneo mbalimbali nchini na kwenye mipaka yetu kwa kushirikiana na mamlaka zinazohusika ili kuwakamata wote wanaojihusisha na biashara hizi na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news