Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Ardhini (LATRA) imetangaza kuanza kwa matumizi ya Tiketi za Kieletroniki kwenye Mabasi yanayokwenda Mikoani na kwa watakaoshindwa kufanya hivyo wasitishe kutoa huduma kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Maamuzi haya yanasimamiwa na Kanuni ya 4(2)(c); Leseni ya kusafirisha abiria itatolewa kwa muombaji aliyesajiliwa kwenye mfumo wa tiketi za kielektroniki ulioidhinishwa na Mamlaka.
Pia, Kanuni ya 24(b)(d); Msafirishaji mwenye leseni ya kusafirisha abiria wa masafa marefu ahakikishe anatoa tiketi za kielektroniki kwa abiria.
LATRA imesema, kupitia mfumo huu, Wananchi watatumia simu kukata tiketi jambo litakaloepusha wizi, ulanguzi wa tiketi na adha za wapiga debe. Pia, unalenga kukomesha vitendo vya upandishaji holela wa nauli hasa kipindi cha mwisho wa mwaka.
Tags
Habari