Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Y . Ndugai (Mb) anasikitika kutangaza kifo cha Mhe. Martha Jachi Umbulla aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM), kilichotokea katika Hospitali ya HCG Mumbai,India alipokuwa anapatiwa matibabu siku ya Jumatano tarehe 21 Januari, 2021 saa 7 usiku kwa saa za India, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa Ofisi ya Bunge leo Januari 21, 2021 jijini Dodoma.
“Nimepokea kwa mstuko na masikitikomakubwa taarifa za kifo cha Mhe. Martha Umbulla. Natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, Waheshimiwa Wabunge na wananchi wa Mkoa wa Manyara. Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,”amesema Mhe. Spika.
Pia ameongeza kuwa, Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.
Tags
Habari