Mtanzania Ibrahim Mgendera atwaa ubingwa wa Mabara wa WBF

Mwanamasumbwi Ibrahim Mgendera (Ibrah Class) amefanikiwa kutwaa ubingwa wa Mabara wa WBF uzito wa Super Light baada ya kumshinda Dennis Mwale wa Malawi kwa alama za majaji wote katika pambano la raundi la 12 usiku wa Januari 29, 2021 ukumbi wa Next Door Arena, Masaki jijini Dar es Salaam, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Mgendera ameshinda pambano la 26 tangu aanze ngumi za kulipwa Juni 26, mwaka 2010, kati ya hayo 11 ameshinda kwa KO, wakati mengine sita amepigwa, matatu kwa TKO.

Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa alikuwepo ukumbini na akamvisha mwanamasumbi huyo taji hilo jipya ambalo linafanya awe na mikanda minne jumla, mingine WPBF, GBC na AAC (All Africans Champion).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news