Naibu Waziri Gekul atembelea Wakala wa Maabara ya Veterinari

Kulia ni Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama, Imani Sichwale.Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu, Wakala ya Maabara ya Veterinari (TVLA), Dkt. Stella Bitanyi (kulia) akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (katikati) alipotembelea Kituo cha Wakala hiyo kilichopo Wilayani Kibaha, Mkoani Pwani Januari 11, 2021. Kushoto ni Kaimu Msajili, Bodi ya Nyama, Imani Sichwale. 
Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha TANCHOICE, Selo Luwongo (wa pili kutoka kushoto) akimuonesha Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (wa pili kulia) maroli yaliyopakiwa minofu ya nyama ya mbuzi zaidi ya Tani 40 kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi alipotembelea Kiwanda hicho Januari 11, 2021.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu, Wakala ya Maabara ya Veterinari (TVLA), Dkt. Stella Bitanyi akimuonesha Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul moja ya chanjo wanazozalisha alipotembelea Kituo cha Wakala hiyo cha kutengeneza chanjo kilichopo Wilayani Kibaha, Mkoani Pwani Januari 11, 2021.
Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha TANCHOICE, Selo Luwongo (kushoto) akimuonesha Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (wa tatu kutoka kushoto) mbuzi waliochinjwa na kuhifadhiwa katika chumba chenye baridi kali kwa ajili ya kusafirishwa kuuzwa nje ya nchi. Gekul alitembelea kiwanda hicho kilichopo Wilayani Kibaha, Mkoani Pwani Januari 11, 2021.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news