Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Joseph Magufuli ameitangaza Halmashauri ya Mji Kahama kuwa Manispaa wakati wa ziara yake mkoani Shinyanga, anaripoti Anthony Ishengoma (Shinyanga).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama mjini Kahama mkoani Shinyanga baada ya kuweka jiwe la msingi leo Alhamisi Januari 28, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine akiweka jiwe la msingi la mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kahama eneo la Malunga mjini Kahama mkoani Shinyanga leo Alhamisi Januari 28, 2021.

Ziara ambayo imelenga kujionea shughuli za maendeleo mkoani humo na kuweka mawe ya Msingi katika Jengo la Utawala la Halmashauri ya mji huo na jengo la wagonjwa wa nje la Hospitali ya Mji Kahama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kahama eneo la Malunga mjini Kahama mkoani Shinyanga baada ya kuweka jiwe la msingi leo Alhamisi Januari 28, 2021.
Uamuzi huo pia ulichagizwa na hatua ya Halmashauri ya Kahama kutoa ardhi bure ili kuwavutia wawekezaji wa ndani jambo ambalo limemwezesha mwekezaji wa ndani, Bw. Muhoja Nkwabi kufungua kiwanda kikubwa cha vinywaji na usindikaji wa vyakula.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kahama eneo la Malunga mjini Kahama mkoani Shinyanga baada ya kuweka jiwe la msingi leo Alhamisi Januari 28, 2021.
Rais Magufuli ameitaja Halmashauri ya Mji Kahama kuwa Halmashauri ya mfano hapa nchini na kupongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Bw. Anderson Nsumba kwa kufanya kazi nzuri za kuendesha miradi mbalimbali kwa kutumia mapato ya ndani.
Pamoja na kuipandisha hadhi Halmashauri ya Mji Kahama kuwa Manispaa pia ametoa msamaha kwa Mkurugenzi Halmashauri hiyo kwa kosa la kununua gari la kifahari na kutaka arudishiwe gari hilo, lakini asiendelee tena na tabia ya hiyo kutumia fedha nyingi katika manunuzi ya magari kama hayo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo kabla ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama eneo la mjini Kahama mkoani Shinyanga leo Alhamisi Januari 28, 2021.
Akiongea na wananchi wa Halmashauri ya Mji Kahama, Rais Magufuli amemwagiza Waziri wa Afya, Bi. Doroth Gwajima kuipandisha hadhi ya Hospitali ya Halmashauri ya Mji Kahama ili iendane na hadhi ya Hospitali za Manispaa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine akiweka jiwe la msingi la mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama eneo la mjini Kahama mkoani Shinyanga leo Alhamisi Januari 28, 2021.
Rais Magufuli pamoja na masuala mengine amewataka wananchi kote nchini kuzalisha chakula kwa wingi ili hapo baadae waweze kujipatia mapato kutokana na nchi jilani ya Tanzania kujifungia kwa kuofia corona na hivyo kutoweza kuzalisha chakula cha kutosha hivyo kuwa fursa kwa watanzania kuuza mazao yao nchi za nje.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine akiweka jiwe la msingi la mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama eneo la mjini Kahama mkoani Shinyanga leo Alhamisi Januari 28, 2021.
Aidha, Rais Magufuli amemwagiza Waziri wa Viwanda na Biashara pamoja na Waziri mwenza wa Kilimo kuhakikisha wanaweka utaratibu utakaowawezesha wakulima mkoani Shinyanga kuuza mazao yao kwa faida baada ya Mbunge wa Kahama, Jumanne Kishimba kudai mkoa huo unahifadhi kubwa ya mchele imbayo imekosa wanunuzi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bi.. Zainab Telack katika salamu zake za Mkoa wa Shinyanga kwa Rais Magufuli ameomba Wizara ya Viwanda na Biashara kuruhusu Mkoa wa Shinyanga kubadili matumizi ya eneo la kiwanda cha nyama kugaiwa kwa wawekezaji kutokana na eneo hilo kukaa bila matumizi, lakini pia kiwanda hicho kukosa wawekezaji kwa sasa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari na wauguzi baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama eneo la mjini Kahama mkoani Shinyanga leo Alhamisi Januari 28, 2021. (Picha zote na Ikulu).
Aidha, Bi. Telack ameongeza kuwa, mkoa wake utaendelea kutoa mchango mkubwa kwa Rais Magufuli katika jitihada kubwa anazozifanya kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania.
Rais Magufuli katika ziara yake hiyo tayari ameweka jiwe la msingi katika jengo la Utawala la Halmashauri ya Mji Kahama, Kiwanda cha Usindikaji wa Chakula cha KOM Group of Companies, Jengo la Wagonjwa wa Nje na anatarajia kufungua mradi wa maji Kagongwa Isaka.
Tags
Habari