Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 17 Januari, 2021 ameungana na Waumini wa Kanisa Katoliki la Bikira Maria, Parokia ya Chato Mkoani Geita kusali Misa Takatifu (Dominika ya 2 ya Mwaka B) iliyoongozwa na Paroko wa Parokia hiyo, Padre Henry Mulinganisa, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Joseph Magufuli akisali leo kanisani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakijumuika na waumini wengine wa Kanisa Katoliki la Bikira Maria Parokia ya Chato katika Ibada ya Jumapili ya Dominika ya pili iliyofanyika Chato mkoani Geita leo tarehe 17 Januari 2021. (Picha zote na Ikulu).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakishiriki Sakramenti Takatifu katika Ibada ya Jumapili ya Dominika ya pili iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita leo tarehe 17 Januari 2021. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waumini wa Kanisa Katoliki la Bikira Maria Parokia ya Chato katika Ibada ya Jumapili ya Dominika ya pili iliyofanyika Chato mkoani Geita leo tarehe 17 Januari 2021.
Mhe. Rais Magufuli ametoa wito kwa Waumini hao na Watanzania wote kwa ujumla kuendelea kumtukuza na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa baraka zake kwa Taifa na hasa kwa kuepusha janga la ugonjwa wa Corona (Covid -19) nchini Tanzania ilihali ugonjwa huo ukiendelea kusababisha vifo vya maelefu ya watu katika nchi nyingine duniani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Paroko wa Kanisa Katoliki la Bikira Maria Parokia ya Chato Padre Henry Mulinganisa mara baada ya kuzungumza na Waumini wa Kanisa hilo Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia Masista mara baada ya Ibada ya Jumapili ya Pili iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia Vijana wadogo wa Kikatoliki mara baada ya Ibada ya Jumapili ya Pili iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Paroko wa Kanisa Katoliki la Bikira Maria Parokia ya Chato Padre Henry Mulinganisa pamoja na Vijana wadogo wa Kikatoliki mara baada ya Ibada ya Jumapili ya Pili ya Dominika ya pili iliyofanyika Chato mkoani Geita leo tarehe 17 Januari 2021.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimsalimia Paroko wa Kanisa Katoliki la Bikira Maria Parokia ya Chato, Padre Henry Mulinganisa mara baada ya Ibada Kanisani hapo.
Amesisitiza kuwa kutokana na Tanzania kuepushwa na ugonjwa huo, Watanzania wanapaswa kutumia nafasi hii kuchapa kazi zaidi hasa kuzalisha mazao mbalimbali yakiwemo mazao ya chakula kwa ajili ya kuzisaidia nchi ambazo zinashindwa kufanya uzalishaji kutokana na watu wake kufungiwa majumbani (lockdown) na pia kukuza uchumi.
“Sasa hivi mvua zinanyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu, nawaombeni sana ndugu zangu Watanzania tulime mazao hasa ya chakula, tulime kwa wingi ili baadaye tuje kuwasaidia wenzetu ambao wanashindwa kulima kutokana na Corona,”amesema Mhe. Rais Magufuli.
Tags
Habari