Rais Magufuli kuzindua shamba la misitu kilomita 690 Chato

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuzindua shamba la miti la Chato leo Januari 27,2021 katika eneo la Butengo wilayani Chato mkoa wa Geita, anaripoti Robert Kalokola (Diramakini) Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Geita mhandisi Robert Gabriel ( wa pili kulia) Kamishna wa uhifadhi nchini, Profesa Silayo Dos Santos (wa pili kushoto). Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Charles Kabeho. Picha na Robert Kalokola/ Diramakini).

Akizungumza na vyombo vya habari Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel amesema Rais Magufuli atazindua shamba hilo lenye ukubwa wa hekta 69,000 sawa na kilometa za mraba 390.

Mkuu wa Mkoa wa Geita amesema kuwa shamba hilo la Miti ni moja ya Mashamba 23 ya serikali yanayosimamiwa na kuendelezwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS).

Amesema, shamba hili limeanzishwa kutoka sehemu ya eneo la msitu mkubwa wa hifadhi ya Biharamulo-Kahama uliohifadhiwa mwaka 1954 kwa tangazo la serikali namba 292 marekebisho ya mwaka 1959 kwa tangazo la Serikali namba 311.

Mhandisi Robert Gabriel amefafanua kuwa, shamba hilo kitakuwa la pili kwa ukubwa nchi baada ya shamba la miti la Sao Hill lililopo Mafinga Mkoani Iringa lenye ukubwa wa hekta 135,900.

Shamba hilo litatoa ajira,kuchochea uhifadhi,ufugaji wa nyuki, kurudisha uasili,wananchi wataweza kujifunza na kuhifadhi misitu na kuongeza kipato kwa kufanya biashara ya mazao yanayo tokana na msitu huo kama vile asali.

Aidha Msitu huo hutasaidia wnaanchi kufanya kilimo mseto ambacho ni miti pamoja mazao ya chakula au ya biashara ya muda mfupi zitaondoa umaskini wa kipato na uhaba wa chakula.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news