Serikali yatoa wito maalum kwa wazazi, walimu wote Zanzibar

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Dkt. Idrissa Muslim Hija amewatangazia walimu, wazazi na wanafunzi wote kuwa Skuli zote zitafunguliwa Januari 18, 2021 visiwani Unguja na Pemba, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu iliyoonwa na Diramakini, pia amesema kuwa, wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha pili wanatakiwa na wao kuripoti Skuli siku hiyo na walimu wawaingize kidato cha tatu.

"Yakitoka matokeo kwa wanafunzi waliofaulu wataendelea na kidato cha tatu na waliofeli watarudia kidato cha pili.Hivyo walimu wakuu wote mnatakiwa kuwajua wanafunzi wote wasiofanya mtihani na sababu zao ziwe za msingi ili Wizara ikichukua hatua iwe na takwimu sahihi,"ameeleza Katibu Mkuu kupitia taarifa hiyo kama inavyosomeka hapo chini.
MADARASA YAPO TAYARI, huu ni muonekano wa darasa likiwa na baadhi ya samani za kisasa ambazo zimekuwa zikinunuliwa na Serikali ya Zanzibar kuhakikisha watoto wanasomea katika mazingira mazuri. Serikali ya Awamu ya Nane chini ya Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi imeazimia kuendeleza, kuboresha na kuratibu mikakati mipya ya kuinua viwango vya Sekta ya Elimu nchini ikiwa ni hatua moja wapo ya kuunga mkono juhudi za Rais mstaafu wa Awamu ya Saba, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed. 
Mchambuzi wa masuala ya elimu amemueleza Mwandishi Diramakini kuwa, wateule wa Rais katika Wizara ya Elimu Zanzibar na wafanyakazi wengine wanapaswa kuwa na mikakati endelevu ambayo itawezesha kuinua zaidi viwango vya elimu, hiyo ikiwa ni hatua moja wapo ya kuyafanikisha malengo ya Mheshimiwa Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi ya kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora ambayo italeta matokeo chanya kwake na kwa Taifa kwa ujumla.

Amesema kuwa,Rais anaitazama sekta ya elimu kwa ukaribu zaidi kama zilivyo Utalii, Afya, Uchumi na nyinginezo, hivyo watumishi wazembe ambao huko nyuma walipenda kufanya kazi kwa kujuana au mazoea watambue kuwa, wanaweza kutumbuliwa muda wowote.

"Mheshimiwa Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi ni miongoni mwa viongozi ambao ninaweza kusema ni wachache sana katika Dunia hii ambao huwa wanafanya kazi muda wote,hivyo niwaombe ndugu zangu ambao mmepewa dhamana ya kuwatumikia wananchi fanyeni kazi, acheni mizaa, maana kwa kasi ya Mheshimiwa Rais wengi watawajibishwa ili wenye uwezo wachukue nafasi hizo kwa ajili ya kuleta ufanisi kazini na matokeo yaonekane,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news