Simba SC wanatarajiwa kumenyana na Dodoma FC, Februari 2 Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kabla ya kuwavaa Azam FC Februari 7, mwaka huu Uwanja wa
Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam katika mechi zao mbili za viporo za
Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Hiyo ni kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa leo Januari 30, 2021 na Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, Almasi J.Kasongo. |