Uongozi wa Wekundu wa Msimbazi, Simba SC umethibitisha kuachana na kocha wake, Sven Vandenbroeck (pichani juu) ikiwa ni siku moja baada ya kuivusha timu hiyo hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuichaoa FC Platinum mabao 4-0 katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Akiwa na Wekundu wa Msimbazi, Sven amepata mafanikio mbalimbali ikiwemo ubingwa wa Ligi Kuu, kombe la FA, ngao ya jamii.
"Kufuatia hatua hii kocha msaidizi Seleman Matola atakaimu nafasi iliyoachwa na Sven mpaka tutakapowatangazia atakayechukua nafasi hiyo hivi karibuni," imeeleza taarifa hiyo. Kikosi cha Simba kipo Zanzibar kujiandaa na mechi za Kombe la Mapinduzi.
Tags
Michezo