Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeaga mashindano ya Kombe la Mataifa Bingwa Afrika (CHAN) baada ya kutoa sare ya goli 2-2 dhidi ya Guinea katika mchezo uliopigwa Leo Jumatano nchini Cameroon, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Stars ambayo ilikuwa inahitaji ushindi wa aina yoyote ile kufuzu hatua ya robo fainali ilijikuta ikilazimishwa sare hiyo na Guinea Equetorial ambao kwao sare yoyote ilikuwa muhimu leo.
Kwa matokeo hayo,Taifa Stars inaaga rasmi mashindano hayo ikiziacha timu za Guinea Equetorial na Zambia kusonga mbele.
Hii inamaanisha kuwa, Taifa Stars na Namibia wanaaga rasmi katika kundi D ambalo lilikuwa na timu nne.
Aidha, kwa sasa ukanda wa Afrika Mashariki umebakiwa na timu moja pekee kwenye michuano ya CHAN ambao ni Rwanda, baada ya Uganda pia kutolewa awali.
Tags
Michezo