UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO: TAREHE: 22/01/2021
Mikoa ya Songwe, Mbeya, Rukwa, Iringa, Njombe, Ruvuma na Kusini mwa mkoa wa Morogoro: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
.........
Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu,Tabora, Dodoma Singida na Kaskazini mwa mkoa wa Morogoro: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
.........
Mikoa ya Lindi na Mtwara: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.
........
Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia),
Tanga pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba, Kilimanjaro, Manyara na Arusha: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.
.......
ANGALIZO:
VIPINDI VYA UPEPO MKALI UNAOFIKIA KM 40 KWA SAA VINATARAJIWA KATIKA MAENEO YA MWAMBAO WA
ZIWA NYASA.
.........
VIWANGO VYA JOTO, VYA JUA KWA BAADHI YA MIJI HAPA NCHINI:
MJI Kiwango cha juu Kiwango cha chini
cha joto cha joto
ARUSHA 29°C 15°C
D'SALAAM 32°C 24°C
DODOMA 26°C 18°C
KIGOMA 29°C 21°C
MBEYA 26°C 17°C
IRINGA 25°C 17°C
NJOMBE 20°C 13°C
MWANZA 28°C 19°C
TABORA 29°C 18°C
TANGA 31°C 22°C
ZANZIBAR 32°C 25°C
..........
Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 30 kwa saa kwa Pwani yote; kutoka Kaskazini Mashariki
kwa Pwani ya Kaskazini, na kutoka Kaskazini kwa Pwani ya Kusini.
Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Makubwa kiasi.
Matarajio kwa siku ya Jumapili tarehe 24/01/2021: Kupungua kwa mvua katika maeneo ya nyanda za juu Kusini
magharibi na Pwani ya Kusini.
Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 22/01/2021.
Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.
MATARAJIO YA HALI MBAYA YA HEWA
JUMAMOSI: 23/01/2021
ANGALIZO la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mwambao wa Ziwa Nyasa.
UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI
KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI
.........
Athari zinazoweza kujitokeza:
Pamoja na ucheleweshwaji wa baadhi ya shughuli za uvuvi.
.........
Tafadhali zingatia na ujiandae.
........
JUMAPILI: 24/01/2021
ANGALIZO la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mwambao wa Ziwa Nyasa.
.........
UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI
KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI
........
Athari zinazoweza kujitokeza
Pamoja na ucheleweshwaji wa baadhi ya shughuli za uvuvi.
.........
Tafadhali zingatia na ujiandae.