Utabiri wa hali ya hewa wa saa 24 zijazo kuanzia 3:00 usiku wa leo tarehe 23-01-2021 unaletwa na mchambuzi Happiness Mpunza kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).Weather forecast
Weather forecast for the next 24 hours starting 21:00 tonight on today January 23rd, 2021 as presented by analyst Happiness Mpunza from Tanzania Meteorological Authority (TMA).UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO: TAREHE: 23/01/2021
Mikoa ya Kigoma, Katavi, Songwe, Mbeya, Rukwa na Njombe: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
.........
Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu,Tabora, Singida, Ruvuma na Iringa: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
.........
Mikoa ya Dar es salaam, Pwani(ikijumuisha visiwa vya Mafia), Kusini mwa mkoa wa Morogoro, Lindi na Mtwara: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.
........
Mikoa Tanga pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba, Kilimanjaro, Manyara, Arusha na Dodoma: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.
.......
VIWANGO VYA JOTO, VYA JUA KWA BAADHI YA MIJI HAPA NCHINI:
MJI Kiwango cha juu Kiwango cha chini
cha joto cha joto
ARUSHA 28°C 16°C
D'SALAAM 32°C 25°C
DODOMA 29°C 20°C
KIGOMA 29°C 21°C
MBEYA 27°C 16°C
IRINGA 28°C 17°C
NJOMBE 20°C 13°C
MWANZA 29°C 19°C
TABORA 29°C 18°C
TANGA 31°C 22°C
ZANZIBAR 32°C 25°C
..........
Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 30 kwa saa kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini, na kwa kasi ya km 20 kwa saa kutoka Kaskazini kwa Pwani ya Kusini.
Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi madogo hadi Makubwa kiasi.
Matarajio kwa siku ya Jumapili tarehe 25/01/2021: mabadiliko kidogo
Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 23/01/2021.
Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.