UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO: TAREHE: 24/01/2021.
………………..........
Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Songwe, Mbeya, Rukwa, Iringa, Njombe, Kigoma, Tabora, Katavi na Ruvuma: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
.........
Mikoa ya Morogoro, Lindi, Mtwara, Dodoma, Singida, Kilimanjaro, Manyara, Arusha, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Tanga pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.
.......
VIWANGO VYA JOTO KWA BAADHI YA MIJI HAPA NCHINI:
MJI Kiwango cha juu Kiwango cha chini
cha joto cha joto
ARUSHA 28°C 16°C
D'SALAAM 32°C 25°C
DODOMA 28°C 20°C
KIGOMA 29°C 21°C
MBEYA 27°C 16°C
IRINGA 28°C 17°C
NJOMBE 21°C 13°C
MWANZA 29°C 19°C
TABORA 29°C 19°C
TANGA 31°C 22°C
ZANZIBAR 32°C 26°C
..........
Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 20 kwa saa kwa Pwani yote; kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kaskazini kwa Pwani ya Kusini.
Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi madogo.
Matarajio kwa siku ya Jumanne tarehe 26/01/2021: mabadiliko kidogo
Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 24/01/2021.
Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.