Utabiri wa hali ya hewa wa saa 24 zijazo kuanzia saa 3 usiku wa leo tarehe 27-01-2021 unaletwa kwenu na mchambuzi Noel Mlay kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
WEATHER FORECAST
Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kigoma, Tabora, Katavi, Songwe, Mbeya, Rukwa, Iringa na Njombe: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
...............
Mikoa ya Kagera, Geita, Mara na Simiyu: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
................
Mkoa wa Ruvuma: Unatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.
.................
Mkoa wa Mtwara: Unatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.
.................
Mikoa ya Lindi, Dodoma, Singida, Kilimanjaro, Manyara, Arusha, Morogoro, Dar es Salaam, Tanga, Visiwa vya Unguja na Pemba,
Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.
..................
VIWANGO VYA JOTO VYA JUA KWA BAADHI YA MIJI HAPA NCHINI:
MJI Kiwango cha juu Kiwango cha chini
cha joto cha joto
ARUSHA 29°C 14°C
D'SALAAM 32°C 26°C
DODOMA 30°C 20°C
KIGOMA 30°C 20°C
MBEYA 24°C 15°C
IRINGA 25°C 18°C
NJOMBE 22°C 12°C
MWANZA 28°C 19°C
TABORA 29°C 18°C
TANGA 32°C 25°C
ZANZIBAR 33°C 26°C
.................
Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 30 kwa saa kwa Pwani yote; kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kaskazini kwa Pwani ya Kusini.
Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Makubwa kiasi.
Matarajio kwa siku ya Ijumaa tarehe 29/01/2021: Mabadiliko kidogo.
Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 27/01/2021.
Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.