WAZIRI MWAMBE AFANYA MAZUNGUMZO NA MTENDAJI MKUU WA DANGOTE PAMOJA NA WAZALISHAJI WA SUKARI NCHINI

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,amekutana na wazalishaji wa Sukari nchini na kusikiliza changamoto zao ili kuzitatua na kuongeza uzalishaji na kuhakikisha Sukari inapatikana kwa urahisi wakati wote nchini, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Akizungumza na na wazalishaji hao Janauari 29, 2021 jijini Dodoma, Mhe.Mwambe amesema kuwa Serikali inalenga kuongeza uzalishaji wenye tija kwa kutumia teknlojia na miundombinu ya kisasa ya umwangiliaji.

''Leo nimekutana na nyie kwa leongo la kujifunza na kujua changamoto mlizonazo katika uzalishaji wa sukari nchini na waahidi tutazifanyia kazi''amesema Mhe.Mwambe.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,akizungumza na Mtendaji Mkuu na Meneja wa kiwanda cha Dangote nchini Tanzania Bw.Abdullahi Baba aliyemtembelea ofisini kwake Januari 29,2021 jijini Dodoma.

Hata hivyo Mhe.Mwambe amewatoa wasiwasi wazalishaji hao kuwa Serikali itashughulikia changamoto hizo ili kuleta maendeleo na kuongeza uzalishaji zaidi nchini .
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,akiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu na Meneja wa kiwanda cha Dangote nchini Tanzania Bw.Abdullahi Baba mara baada ya mazungumzo ofisini kwake Januari 29,2021 jijini Dodoma.

Awali Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu na Meneja wa kiwanda cha Dangote nchini Tanzania Bw.Abdullahi Baba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news