Waziri wa China atua nchini,atoa milioni 350/- kusaidia VETA Chato

Waziri wa Mambo ya Nje na Mjumbe wa Baraza la Taifa wa China ,Wang Yi ametoa msaada wa fedha za China milioni moja sawa na dola za kimarekani laki moja na nusa ambazo ni shilingi za Kitanzania Milioni 350 kwa ajili ya kuendeleza Chuo cha Ufundi (VETA) cha Chato mkoani Geita, anaripoti Robert Kalokola (Diramakini) Chato.
Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi (kushoto) akiwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Tanzania, Profesa Joyce Ndalichako wakati wakifungua rasmi Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Chato, Geita. (Picha na Robert Kalokola/ Diramakini). 

Akizungumza kwa niamba ya Serikali ya Tanzania, Waziri wa Elimu,Sayani na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema fedha hizo zitatumika kununua vifaa vya mafunzo ya fani ya uvuvi katika chuo hicho.

Awali akitoa taarifa fupi kwa Waziri huyo wa China, Mkurugenzi Mkuu wa Vyuo vya Ufundi nchini (VETA), Pancras Bujuru amesema, chuo hicho cha ufundi kimelenga kuwanufaisha wananchi kwa kuzingatia Chato kuna mbuga za wanyama kama Buringi-Chato,kisiwa Cha Rubondo,shughuli za madini na shughuli ufugaji na uvuvi.

Kwa upande wake, Dkt.Medard Kalemani ambaye ni Waziri wa nishati na Mbunge wa Jimbo la Chato amesema, chuo hicho kitanufaisha watu wa Wilaya ya Chato na mikoa ya jirani.

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa , kitendo cha Waziri Wang Yi kukubali kufungua chuo hicho ni ishara ya mshikamo na urafiki.

Ameongeza kuwa lengo la serikali ya Tanzania ni kujenga chuo kimoja cha ufundi kila wilaya ili kuendana na Malengo ya Maendeleo ya mwaka 2025.

Ndalichako amesema kuwa, serikali itaendelea kujenga vyuo vya ufundi kwa kutumia mapato ya ndani na kwa kushirikishana na nchi marafiki.

Waziri Ndalichako ameishukuru serikali ya China kwa kujenga chuo cha ufundi kimoja katika mkoa wa Kagera ambacho kitasaidia kukuza ujuzi kwa wananchi wa Tanzania.

Aidha, Ndalichako ameiomba serikali ya China kuendesha mafunzo kwa wakufunzi wa vyuo vya ufundi na karakana za vyuo hivyo hapa nchini ili kupata ujuzi zaidi.

Amesema , serikali iko tayari kupokea karakana ambayo China imekubali kujenga Afrika na ingekuwa moja ya sehemu ya chuo cha VETA Chato.

Profesa Ndalichako ameomba serikali ya China kuzitaka taasisi za China zinazofanya kazi hapa nchini kushirikiana na vyuo vya VETA hapa nchimi ili kukuza vipaji.

Waziri wa Mambo ya Nje na Mjumbe wa Baraza la Taifa wa China, Wang Yi amesema kuwa ili Tanzania kufikia maendeleo inahitaji vijana wenye ujuzi.

Wang Yi amesisitiza kuwa nchi ya China itaendelea kusaidia nchi ya Tanzania na Sasa inatoa milioni moja ya China kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya chuo hicho.

Aidha, amesema kuwa,endapo Kuna mahitaji kwa ajili ya chuo hicho, uongozi wa chuo hicho uwasilishe kwa Balozi wa China nchini Tanzania ambaye atakuwepo chuoni hapo.
 
Ameongeza kuwa, Serikali ya Watu wa China imejenga chuo cha ufundi stadi katika mkoa wa Kagera ambacho kitakuwa na uwezo wa kuhudumia wanafunzi 1000 kwa kozi zote. 
 
Waziri Wang Yi amefika nchini kwa ajili ya ziara ya siku mbili katika mkoa wa Geita ambapo amefungua chuo cha Veta Chato.

Kazi nyingine atakayofanya ni pamoja na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli na baadae yeye pamoja na ujumbe wake watafanya mazungumzo na mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikino wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi.

Pia atashuhudia kutia saini mkataba wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Mwanza kwenda Isaka kilomita 341 ambayo mzabuni ni makampuni mawili ya China na atatembelea mwalo wa uvuvi wa samaki wa Chato.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news