Yanga SC yatambulisha makocha wapya wawili

Uongozi wa Yanga SC umetambulisha wafanyakazi wawili ambao wanaingia jumla kwenye benchi la ufundi kuendeleza gurudumu la kusaka ushindi ndani ya uwanja, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Miongoni mwa wale ambao wametambulishwa Januari 27, 2021 ni pamoja na mzawa, Nizar Khalfani ambaye yeye anakuja kuwa kocha msaidizi akichukua mikoba ya Juma Mwambusi ambaye aliomba kujiweka kando kutokana na matatizo ya afya.
Mchezaji wake wa zamani, Nizar Khalfan akitambulishwa Kocha mpya Msaidizi wa Yanga SC.

Khalfan ambaye ni mchezaji wa zamani wa kikosi cha Mtibwa Sugar alikuwa anaifundisha timu ya African Lyon ambayo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza.
Edem Mortotsi akitambulishwa kuwa kocha mpya wa mazoezi ya viungo wa Yanga SC.

Mwingine ambaye ametambulishwa ndani ya benchi la ufundi ni Edem Mortotsi ambaye ni raia wa Ghana yeye anakuja kuwa kwenye benchi la ufundi akiwa ni kocha wa viungo.

Afisa Uhamasishaji wa kikosi cha Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa malengo ya kufanya hivyo ni kuongoze nguvu ndani ya timu hiyo ya Wananchi. Aidha, wanaungana na Kocha Mkuu, Cedric Kaze ambaye ni raia wa Burundi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news