Benki ya NMB yatoa vifaa vya milioni 50/- Singida, Morogoro na Dodoma

Benki ya NMB imetoa vifaa mbalimbali katika sekta ya elimu na afya kwenye wilaya za Mpwapwa mkoani Dodoma, Manyoni na Itigi mkoani Singida pamoja na Morogoro vikiwa na thamani ya shilingi milioni 50, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Vifaa hivyo ni pamoja na meza,viti, madawati pamoja na vitanda kwa ajili ya vituo vya afya mbalimbali, vikiwemo vutanda kwa ajili ya kujifungulia akina mama wajawazito.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mazoezi Lupanga wakisomba viti na meza baada ya Benki ya NMB Kanda ya Mashariki kutoa msaada wa viti na meza 110 kwa shule za sekondari hiyo na Kihonda sekondari.

Katika Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma benki hiyo imetoa madawati 50, vito 50 pamoja na meza 50 vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 15.

Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi akikabidhi vifaa hivyo kwa Mkuu wa Wilaya hiyo Jabir Shekimweri amesema kuwa, NMB imetoa msaada huo ili wanafunzi na waweze kujifunza katika mazingira mazuri.

Aidha, Mlozi alisema kuwa vifaa vilivyotolewa ni kwa ajili ya shule ya Sekondari Matomondo huku ikiwa pamoja na Mabati ya kuezekea kituo cha Afya Kisokwe kilichopo katika Wilaya hiyo.

Akipokea vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya hiyo Shekimweri aliishukuru benki hiyo kwa msaa huo ambao alieleza kuwa utapunguza changamoto zilizopo kwenye shue hizo pamoja na kituo cha Afya.

Aliongeza kuwa, msaada huo utaondoa changamoto ya wanafunzi kukaa chini wakati wa masomo na kuleta uafaulu kwa wanafunzi kwenye masomo yao.

Katika Mkoa wa Singida, benki hiyo imetoa madawati 150 yenye thamani ya sh. Milioni 15 kwa shule tatu za msingi ambazo ni Sanjaranda, Mlowa na Mbugani zote za halmashauri ya Itigi.

Mbali na madawati benki hiyo imetoa vitanda 12 pamoja na magodoro yake yenye thamani ya sh milioni tano kwa ajili ya wodi ya akinamama kwenye kituo cha afya Itigi ambacho kinasaidia kuhudumia wananchi wa eneo hilo na wilaya jirani za Mkoa wa Mbeya na Tabora.

Meneja Benki hiyo Kanda ya Kati Nsolo Mlozi akikabidhi vifaa hivyo alisema kuwa mbali na hivyo NMB imetoa vitanda saba kati ya hivyo vitanda viwili ni kwa jili ya akinamama kujifungulia na mashuka 30 vyote vikiwa na thamani ya Shilingi Milioni tano.

Alisema NMB itaendelea kutoa misaada zaidi kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dk.John Magufuli.

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa ,Jabir Shekimweri (kulia mwisho) akipokea msaada mabati kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati ,Nsolo Mlozi (kushoto kabisa ) kwa ajili ya Zahanati ya Kijiji cha Kisokwe, Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma juzi,NMB ilikabidhi msaada wamadawati 50 kwa ajili ya shule ya msingi Makutupa ,viti 50 na meza 50 kwa ajili ya shule ya sekondari Matomondo pamoja na mabati kwa ajili ya Zahanati ya Kisokwe.

Mkuu wa Wilaya ya Manyoni,Rahabu Mwagisa ameipongeza benki ya NMB kutokana na kuisaidia jamii msaada wa thamani ya sh milioni 25 kwenye sekta muhimu ya elimu na afya .

“Nataka niwapongeze kwa dhati ya moyo wangu benki ya NMB msaada huu miliotoa kwenye Halmashauri hizi mbili umeigusa jamii kutokana na kuipunguzia mzigo serikali,” alisema Mwagisa.

Mbunge wa Jimbo la Manyoni Magharibi,Yahaya Massare alisema misaada inayotolewa na Nmb inasaidia serikali kutekeleza ilani ya uchaguzi yake ya uchaguzi iliyoahidi wakati wa kampeni .

Katika Mkoa wa Morogogo NMB imetoa viti na meza 110 vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 10 kwa ajili ya shule ya sekondari Kihonda na shule ya sekondari Mazoezi Lupanga Kigurunyembe ili kupunguza changamoto ya madawati kwa wanafunzi wa shule hizo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news