CAF yafuta mechi ya Namungo FC dhidi ya Primiero De Agosto ya Angola
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limefuta mechi ya mchujo wa kuwania hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho baina ya wenyeji Primiero de Agosto na Namungo FC ya Tanzania iliyopangwa kuchezwa kesho Uwanja wa Novemba 11 Jijini Luanda.