Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli amesema Wakristo ambao wapo katika kipindi cha Kwaresma na Waislamu ambao wanakaribia kuingia katika kipindi cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, waendelee kumuomba Mungu kwani pamoja na jitihada za kibinadamu za kukabiliana na ugonjwa wa Corona, Mungu ndiye muweza wa yote na husimama kwa kila jambo.