Ni mwendelezo wa kombe la FA, ambapo leo Februari 27, Yanga SC imeshuka dimbani kuvaana na Ken Gold, katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
KUHUSU KEN GOLD
Hii timu inamilikiwa na Keneth Mwakyusa (Ken) ambaye ni mfanyabiashara wa madini wilayani Chunya mkoani Mbeya yaliko makao makuu ya timu hiyo.
Ken aliinunua timu ya Gipco FC kutoka Geita iliyokuwa ikishiriki Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambayo ilibadilishwa jina na kuitwa Ken Gold, jina la timu yake ambayo awali ilikuwa ikishiriki ligi ya wilaya.
Kocha wa Ken Gold ni Salvatory Edward Augustin ambaye ni mchezaji wa zamani wa Yanga na amewahi pia kuwa sehemu ya benchi la ufundi la Yanga.
Jana Simba SC imetinga hatua ya 16 Bora michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya African Lyon Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Simba SC yalifungwa na Ibrahim Ajibu mawili dakika ya 10 na 44 na Mzimbabwe Perfect Chikwende dakika ya 63, wakati Meddie Kagere alipiga nje penalti dakika ya 21 kuwakosesha Wekundu wa Msiimbazi bao lingine.